Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 21, 2016

LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA KESHO, MCHEZAJI AMBAYE HANA LESENI KUTOCHEZA


WACHEZAJI ambao hawana leseni hawataruhusiwa kucheza ligi daraja la kwanza kuanzia mzunguko wa tano unaotarajia kuanza  kesho.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas, alisema Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania imeagiza makamishna na wasimamizi wa vituo kuhakikisha mchezaji ambaye hana leseni hachezi
“Kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (16),  ‘Wachezaji wote watatambulika kwa kutumia leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na TFF. Mchezaji yoyote ambaye hatakuwa na leseni hataruhusiwa kucheza katika mchezo husika.”, alisema Lucas
Lucas alisema shirikisho  lilitoa kipindi cha dharura kutumia leseni za muda wakati leseni za msimu zikiandaliwa hivyo leseni zipi tayari lakini viongozi wa timu hawajaenda kuzichukua TFF.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza, michezo ya Kundi A leo itakuwa ni kati ya Pamba ya Mwanza na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kutakuwa na Kiluvya United ambayo itacheza na Mshikamano.
Jumatatu katika kundi hilo, Friends Rangers itacheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Karume na Jumanne Polisi Dar itacheza na Ashanti United ya Ilala, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya Warriors ya Mbeya na Coastal Union ya Tanga; Kemondo itacheza na Mlale na Polisi Moro itacheza na Kurugenzi ya Iringa wakati kesho KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam itacheza na Mji Njombe.
Kundi C michezo yote minne itachezwa leo, Singida United itacheza na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Namfua, Singida; Rhino itapambana na Alliance ya Mwanza kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora huku Mgambo JKT itakuwa mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.