Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 9, 2016

RATIBA LIGI KUU ENGLAND DIMBANI JUMAMOSI, MECHI YA KWANZA NI DABI YA MANCHESTER, MAN UNITED vs MAN CITY


BAADA kupumzika kwa Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa, LIGI KUU ENGLAND, EPL, itarejea tena kilingeni Jumamosi Septemba 10 na Mechi ya kwanza kabisa ni Dabi ya Manchester kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester City.
Mechi hii itachezwa Uwanjani Old Trafford na kuzikutanisha Timu ambazo, pamoja na Chelsea, ndizo pekee zilizocheza Mechi zao 3 na kushinda zote na hivyo kuwa kileleni.
Mechi hii, ambayo itachezwa Saa 8 na Nusu Mchana na kusimamiwa na Refa Mark Clattenburg, inawakutanisha Mameneja wapya kwa Klabu zao ambao ni Mahasimu tangu huko Spain walipozioongoza Real Madrid na Barcelona.
Hivi sasa Jose Mourinho, aliekuwa Real Madrid, ni Meneja wa Man United na Pep Guardiola, aliekuwa Barcelona ni Meneja wa Man City.
Mara baada ya mtanange huo wa Dabi, Saa 11 Jioni, zipo Mechi nyingine 6 za EPL ikiwemo ile ya Arsenal kucheza Nyumbani na Southampton na Tottenham kuwa Ugenini kucheza na Stoke City.
Jumamosi itafungwa na Mechi ya Saa 1 na Nusu Usiku huko Anfield ambako Liverpool watacheza na Mabingwa Watetezi Leicester City.

Jumapili ipo Mechi 1 kati ya Swansea City na Chelsea na Jumatatu Usiku pia ipo Mechi moja huko Stadium of Light kati ya Sunderland na Everton.
LIGI KUU ENGLANDRATIBA:
Jumamosi Septemba 10

14:30 Man United v Man City
17:00 Arsenal v Southampton
17:00 Bournemouth v West Brom
17:00 Burnley v Hull
17:00 Middlesbrough v Crystal Palace
17:00 Stoke v Tottenham
17:00 West Ham v Watford
19:30 Liverpool v Leicester
Jumapili Septemba 11
18:00 Swansea v Chelsea
Jumatatu Septemba 12
22:00 Sunderland v Everton