Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao zote za Kilimanjaro Queens zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza limefungwa na Asha Rashid dakika ya 22, Bao la pili lilifungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30 huku
Bao la tatu lilikuwa la kujifunga wao wenyewe baada ya mabeki wa Burundi kujichanganya na mchezaji Niyonkulu Saidauze kwenye harakati za kutaka kuokoa mpira kwenye eneo hatari dakika ya 33. Hadi dakika 90 zinamalizika Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wababe kwa kutoka na ushindi wa bao 3-0. Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliokuwa ni moja ya Timu zote mbili kujiandaa na Michezo ya CECAFA Nchini Uganda. Na Kesho Timu zote mbili zinaelekea jijini Jinja, Nchini Uganda.
Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake Burundi kilichoanza leo dhidi ya Kilimanjaro Queens.Timu ya Wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens wakiomba kabla ya Mechi kuanza.
Burundi wakipanga mbinu na kuwabana Kilimanjaro Queens punde kabla ya kipute kuanza
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akisalimiana na waamuzi
No comments:
Post a Comment