Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 22, 2016

JESHI STARS WANAWAKE NA WANAUME ZATWAA UBINGWA WA KLABU BINGWA WAVU BARA
TIMU za mchezo wa wavu za Jeshi, wanawake na wanaume, wametwaa ubingwa wa klabu bingwa kwenye mashindano yaliyokuwa yalifanyika Pwani tangu Agosti 19-22.
Akizungumza na gazeti hili, kocha wa timu ya Jeshi Stars, Lameck Mashindano alisema anashukuru wachezaji wake kujituma na hatimaye kuibuka mabingwa wa klabu bingwa bara kwa kuzifunga timu za Magereza.
"Magereza ni timu nzuri na awali walianza vema kwani kipindi cha kwanza walikuwa wanaongoza, tuliporudi tulianza kwa kasi na mabadiliko niliyofanya yalisaidia kubadilisha mchezo", alisema Mashindano.
Pia Mashindano alisema timu hizo zilifanikiwa kutoa wachezaji bora wanne, mmoja kwutoka kwenye timu ya wanaume ambaye ni Jackson Goodluck, na wanawake ni Neema Ngowi, Yasinta Remmy na Dorine Kobelo.
Jeshi Stars wanaume waliibuka bingwa baada ya kuifunga Magereza wanaume kwa seti 3-2 na Jeshi stars wanawake waliifunga Magereza wanawake seti 3-0.