Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 22, 2016

TIKETI ZA ELEKTONIKI KUANZA RASMI SEPTEMBA 4 UWANJA WA TAIFA



TIKETI za kilectroniki Uwanja wa Taifa, zitaanza kutumika Septemba 4  baada ya kazi ya kufunga mashine kumalizika.
Mashine hizo zitafungwa kwenye mageti ya kuingilia uwanja wa Taifa ambapo mtu mmoja atahudumiwa kwa sekunde mbili huku masine 20 zikifungwa kwenye mageti yote ya kuingilia uwanja huo na  dakika 180 zikitosha kuwahudumiwa mashabiki wote watakaohudhuria.

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Daktari, Elisante Ole Gabriel amesema kazi hiyo inafanya kazi hiyo ya kufunga mfumohuo inafanywa na kampuni ya Selcom itakabidhiwa kwa Waziri Nape Nnauye Septemba 4.

Katibu huyo alisema kuwa mashine hizo zimechelewa kuanza kutumika kwasababu zilikuwa zikifanyiwa majaribio ya kuweza kuwahudumia watu wengi kwa wakati mmoja ili kupunguza usumbufu kwa wapenzi wa soka.
Naye Waziri Nape alisema mfumo huo utasaidia Serikali kupata mapato kulinganisha na utaratibu wa tiketi za kukata za kawaida  ambao zilikuwa ukiwanufaisha watu wachache ambao aliwataja kwa jina la 'Makomandoo'.

"Kwa mfumo huu sasa Serikali itaingiza mapato makubwa kupitia kodi itakayokatwa kwa kila tiketi itakayonunuliwa na wale wanaojiita Makomandoo watafute kazi nyingine ya kufanya" alisema Nape.

No comments:

Post a Comment