Anacheeeka! Muimbaji mashuhuri wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto au Mjomba akisalimiana na Rais Dr Pombe Magufuli kwenye Uwana wa Ndege jjjini Dar es Salaam jana. Kulia kwa mjomba ni Katibu Mkuu wa CCM Ibrahim Kinana. |
Na Mwandishi Wetu
RAIS Dr John Pombe Magufuli amefurahishwa na kibao
cha muimbaji mashuhuri wa mashahiri nchini, Mrisho Mpoto cha Sizonje, ambacho
kinazugumzia hali halisi ya nchi na mambo mengine, imeelezwa.
Rais
Magufuli alikutana ana kwa ana na muimbaji huyo jana kwenye Uwanja wa
Ndege wazamani jijini Dar es Salaam wakati akirejea kutoka
katika ziara ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo Mwanza,
ambako alihutubia juzi kwenye
viwanja vya Furahisha.
Mrisho Mpoto au Mjmba akicheza ngoma wakati akisubiri kutua kwa Rais Dr Pombe Magufuli jana akitokea Mwanza. |
Mpoto alisema jana kuwa alikwenda Uwanja wa Ndege
akiwa na kundi lake la ngoma lililoko chini ya Mjomba Theatre, ambapo alikuwa akipiga
ngoma, kucheza na nyoka na sarakasi, na Rais baada ya kuteremka katika
ndege, alianza kutembelea vikundi vya
burudani na moja kwa moja alikwenda kwa Mjomba.
Baada ya kushuhudia kidogo maonesho ya Mjomba, Magufuli
alimuita msanii huyo na kusalimiana naye kabla ya kuanza kuzungnumza naye na
hapo ndipo alipomueleza kuwa, kibao cha
Sizonje ndio chaguo lake kubwa, kwani anakipenda
sana.
Kwa mujibu wa Mpoto, Rais alisema kuwa Sizonje ndio
kibao chake bora kabisa, ambapo alimsifu Mjomba kwa kibao hicho, ambacho
kimejaa mafumbo mengi yanayowafanya watu kuwa na mawazo tofauti.
Alisema Rais Magufuli alimuambia anaipenda nyimbo
yake ya mwisho, ambayo ni Sizonje na akuyatamka baadhi ya maneno yaliyomo
katika kibao hicho.
“Nasikiliza
sana nyimbo zako, ila huu wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku,…
mwanzo nilipata tabu sana kuuelewa, lakini sasa hivi, aaah nimeuelewa vibaya
mno, “alisema Mjomba akimkariri Rais Maufuli.
Mpoto anajulikana kwa vibao vyake, ambapo aliwahi
kuimba kibao cha Mjomba, ambacho wengi walitafsiri kuwa alimuimba Rais wa awamu
ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, lakini alipoulizwa mjomba ni nani, Mpoto
alisema: Ni kaka yake mama.”
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baadae
uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa amefarijika sana kwa maneno ya busara kutoka
kwa Rais, inanitia moyo sana kujua kuwa
Rais ni shabiki wangu mkubwa na yeye mwenyewe kwa maneno yake amesema huwa
anasikiliza nyimbo zangu akiwa Ikulu, “alisema Mjomba.
No comments:
Post a Comment