Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 13, 2016

PAUL POGBA KUIKOSA MECHI YA KWANZA JUMAPILI MAN UNITED v BOURNEMOUTH

MCHEZAJI MPYA wa Manchester United Paul Pogba ataikosa Mechi ya kwanza kabisa ya Manchester United ya Ligi Kuu England Ugenini Jumapili na Bournemouth kwa sababu atakuwa kifungoni.
Pogba, mwenye Miaka 23, alihamia Man United kutoka kwa Mabingwa wa Italy Juventus Siku kadhaa zilizopita na kuwa Mchezaji wa Bei Ghali kabisa Duniani baada ya kununuliwa kwa Dau la Pauni Milioni 89.

Lakini, FA, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwa Pogba alizoa Kadi za Njano mbili huko Italy kwenye Michuano ya Coppa Italia akiichezea Juventus Msimu uliopita na hivyo kupaswa kutumikia Kifungo cha Mechi 1.
FA imethibitisha Kifungo hicho kitatumikiwa kwenye Mechi dhidi ya Bournemouth.

Mechi ya kwanza kwa Pogba kuichezea Man United inaweza kuwa Ijumaa Agosti 19 Uwanjani Old Trafford wakati Man United ikicheza na Southampton kwenye Ligi Kuu England.