Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 13, 2016

JOSE MOURINHO AOMBWA MSAMAHA SAKATA LA BASTIAN SCHWEINSTEIGER.

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho ameombwa msamaha na yule aliedai Siku kadhaa nyuma kwamba aswekwe Jela kwa ‘kumyanyasa’ Bastian Schweinsteiger.

Hayo yalitamkwa na Dejan Stefanovic kutoka Slovenia ambae ni Mwanachama wa FifPSro, Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji Soka Profeshenali.
Kauli hiyo ya Dejan Stefanovic ilikuja baada ya Schweinsteiger, Kiungo wa Mabingwa wa Dunia Germany mwenye Miaka 32 aliesaini Man United Mwaka Jana kwa Mkataba wa Miaka Mitatu na kucheza Gemu 31 lakini Msimu huu, chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho kutupwa kwenye Kikosi cha Rizevu kufanya nao mazoezi.
Stefanovic alidai huo ni ‘unyanyasaji’ na kuomba adhabu ya juu ambayo ni Kifungo cha Miaka Mitatu Jela!’

Stefanovic, ambae ni Mwanasheria na pia ni Rais wa Chama cha Wachezaji Soka na Masapota huko Slovenia, amedai Mourinho anataka kumkatisha tamaa Schweinsteiger.

Lakini huko England, Chama cha Mameneja wa Ligi, LMA [League Managers' Association] kilisema matamshi hayo ya Stefanovic hayakustahili na hii Leo LMA imetangaza kuwa Dejan Stefanovic amemtaka radhi Mourinho.