Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 16, 2016

MENEJA BILIC ASEMA 'COSTA ALIPASWA KUPEWA KADI NYEKUNDU


Diego CostaMENEJA wa West Ham United Slaven Bilic amesema Straika wa Chelsea Diego Costa alistahili Kadi Nyekundu kwenye Mechi ambayo West Ham walichapwa 2-1 na Chelsea Jana Usiku huko Stamford Bridge.
Costa ndie aliefunga Bao la Pili na la ushindi kwa Chelsea katika Dakika ys 89.
Lakini, kabla ya hapo, akiwa tayari ashatwangwa Kadi ya Njano, Costa alimchezea Rafu Kipa wa West Ham Adrian lakini Refa Anthony Taylor alitoa Frikiki bila ya kumpa Kadi ya Njano ambayo ingemfanya astahili Kadi Nyekundu na kutolewa nje.
Kubaki kwa Costa Uwanjani kulimfanya ampe Meneja wao mpya Antonio Conte ushindi wao wa kwanza katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Akiongea na Sky Sports, Bilic alisema: "Tayari alikuwa na Kadi na alicheza rafu na sidhani ni kusudi lakini alichelewa na alipaswa kupewa Kadi nyingine!"

Kwenye Mechi hiyo, West Ham walipata pigo baada kulazimika kumtoa nje Mchezaji wao mpya kutokana Ghana, Andre Ayew, alieumia Pajani katika Dakika ya 35.

LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17

Ijumaa Agosti 19
22:00 Man United v Southampton
Jumamosi Agosti 20
14:30 Stoke City v Man City
17:00 Burnley v Liverpool
17:00 Swansea v Hull
17:00 Tottenham v Crystal Palace
17:00 Watford v Chelsea
17:00 West Brom v Everton
19:30 Leicester City v Arsenal
Jumapili Agosti 21
15:30 Sunderland v Middlesbrough
18:00 West Ham v Bournemouth