Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 16, 2016

MALINZI ACHAGULIWA TENA KUONGOZA CHAMA CHA SOKA KRFA

Na Faustine Ruta, Bukoba
Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu kwenye ukumbi wa Hotel ya Optima iliyopo Bunazi Misenyi ambapo chama hicho kilichokuwa kinaongozwa na Wajumbe 22 kumteua Jamal Emil Mlinzi tena kukiongoza chama hicho kwa kura za Ndiyo.
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera Bw. Jamal Emil Malinzi ambaye amechaguliwa tena kikiongoza Chama hicho kwa mara nyingine kwa Miaka 4. 
Akiongea na Mtandao huu wa Bukobasports amesema kwa sasa wameanza na mkakati wa kuboresha Uwanja wa Kaitaba kwa kuuwekea Nyasi bandia na kuongeza idadi ya Majukwaa ili uweze kutumika kwa Michezo ya Kimataifa. Pia Chama cha mpira wa miguu Mkoa kimeomba Viwanja kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo na Uwanja wa kwa Ufadili wa FIFA jambo ambalo kimsingi linawezekana kila Mtu akitimiza wajibu wake. 
Pamoja na hayo aliomba kupitia mkutano huo kuviomba Vyama vyote vya Wilaya kuomba maeneo ya kujenga Viwanja vya mpira wa miguu kwenye Halmashauri zao husika. 

Mwisho aliwashukuru wote kwa nafasi zao na kuwaomba ushirikiano wa hali na mali ili Mkoa wa Kagera uweze kuongeza Timu zingine  katika Ligi kuu Vodacom na Madaraja mengine.
Kwa Makini sana wakimsikiliza Mjumbe
Hussein na Abdulzack Malick Sudi Tibabimale(kushoto) akisikiliza neno kwa makini kutoka kwa Mjumbe


Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera Bw. Jamal Emil Malinzi ambaye amechaguliwa tena kikiongoza Chama hicho kwa mara nyingine kwa Miaka 4 akipongezwa na Baadhi ya Wajumbe na Viongozi mbalimbali kwenye Ukumbi huo wa Optima mara baada ya kushinda.


Viongozi (Kamati Tendaji) waliochaguliwa leo kukiongoza Chama cha Soka Kagera KRFA

No comments:

Post a Comment