KAMATI ya
Rufani za uchaguzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetengua maamuzi ya
kamati ya uchaguzi ya TFF kuhusu uchaguzi wa Chama cha Soka cha Kinondoni, KIFA
na kudai kamati hiyo imekiuka katiba ya TFF.
Akizungumza wandishi wa habari, Mwenyekiti wa
kamati ya rufani za uchaguzi, Wakili
Julius Lugaziya alisema kamati ya uchaguzi ya TFF kikanuni haina mamlaka ya kutengua,
kusitisha uchaguzi wa vyama vya wilaya kwani siyo mwanachama wa TFF.
"Kamati ya rufani ilipokea rufani toka kwa Thomas
Manzanda ikasikiliza pande mbili ambayo ni TFF iliwakilishwa na wakili Edward
Muga na Manzanda ikagundua kuwa rufani imekuja nje ya muda lakini kutokana na
mamlaka iliyonayo ikaona kuna jambo la muhimu hivyo ikaendela
kuisikiliza", alisema Lugaziya.
Wakili Ligaziya alisema kamati imetengua maamuzi ya
kamati ya uchaguzi ya TFF hadi rufaa ya Thomas Manzanda itakaposikilizwa na
kamati ya rufani ya DRFA ambayo imepewa siku 14 tangu kamati hiyo ilipotoa
maamuzi Agosti 15.
Kabla ya kusoma maamuzi hayo Mwenyekiti Lugaziya alisema mwendeno wa rufaa hiyo
ulivyokuwa na kusema Wakili wa TFF, Edward Muga alijaribu kuishawishi kamati
yake kuwa maamuzi ya kamati ya uchaguzi yalikuwa sahihi lakini Lugaziya akasema
kamati hiyo imekiuka kanuni za TFF ibara 52 kifungu cha sita.
Wakili Lugaziya alisema kamati ya uchaguzi ina mamlaka
ya kuingilia uchaguzi wa wanachama wa TFF endapo kuna malalamiko katika
mchakato wa kuwapata wagombea, rushwa, haki ya kutosikilizwa kwa wagombea
(natural justices) na endapo matokeo yatakuwa ya kughushi.
Wakili Lugaziya alifika mbali na kudai Kamati ya
uchaguzi na TFF haikupata malalamiko bali ilipata nakala ambayo ilitumwa kwa
kamati ya rufaa hivyo ilikaa kama kamati ya rufani mamlaka ambayo haikuwa nayo
.
Uchaguzi wa Chama cha Soka cha Kinondoni ulifanyika
kwa mara ya kwanza Juni 12 lakini kamati ya uchaguzi ya KIFA ikatengua matokeo
yake baada ya kugundua kura zimezidi idadi ya wapiga kura, ukarudiwa tena Julai
18 ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilitengua na kuagiza uchaguzi urudie na
nidhamu zichukuliwe kwa watu mbalimbali
kinyume na kanuni za TFF.
Baadae ya kutengua matokeo ya Julai 18, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF iliitisha kikao cha maridhiano kwa kutumia barua ambayo haikuwa
yake na idadi ya watu waliotakiwa kufika bila kusema mkutano utafanyika wapi
wala muda wa mkutano na bila kuwashirikisha walioandika barua
Pia Kamati ilipitisha uamuzi wa kufanyika uchaguzi upya
huku ikijua kuwa Manzanda amekata rufaa DRFA
kwa mujibu wa kanuni na katiba
No comments:
Post a Comment