Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 19, 2016

MAVUGO APATA ITC, KESHO KUIVAA NDANDA TAIFA
KLABU ya Simba imepata uhammisho wa kimataifa  (ITC) za wachezaji wake wa kigeni Laudit Mavugo na Frederic Blagnon leo mchana baada ya kukamilisha uhamisho wao.
Katika taarifa iliyopostiwa kwenye mitandao na katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kihemele inasema ITC  zimetua nchini leo mchana kutoka katika mashirikisho ya soka ya Burundi na Ivory Coast.
Blagnon Fredric Goue ametokea klabu ya Africa Sports ambao ni wapinzani wa jadi wa ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Kupatika kwa hati hizo kunamaliza utata wa uhamisho wa Mavugo ambaye kulitokea kwa maneno toka kwa uongozi wa klabu ya Vital’O kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja jambo ambalo lilikanushwa na Mavugo.