Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 19, 2016

KESSY ATAKIWA KUILIPA SIMBA MAMILIONI

Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji imepitisha usajili wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha jina la mchezaji Hassan Kessy kuichezea Young Africans. Hii ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas. 
Kamati hiyo iliyoketi jana chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Richard Sinamtwa imemtaka beki huyo kuilipa klabu ya zamani, Simba milioni 120 kwa kuvunja Mkataba.
Habari za ndani kutoka TFF zimesema kwamba Kamati imejiridhisha kwamba Kessy alivunja Mkataba na Simba kinyume cha utaratibu hivyo anapaswa kuilipa Simba.
Na habari zaidi zinasema kwamba, katika Mkataba wake na Simba, wote klabu na mchezaji walikubaliana atakayeuvunja atalipa dola za Kimarekani 60,000 zaidi ya Sh. Milioni 120,000 za Tanzania.
Kessy alisajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa Mkataba wa miaka miwili akilipwa Sh. Milioni 20.