KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari
za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri
Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa wa kamati hiyo. Majina
yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online),
Jane John (TBC), Baruani Muhuza (Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid
Kitenge (E-FM Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda
(Clouds Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
Kamati inaweza kuongeza wajumbe wengine au kupunguza
kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na
sekreterieti ya TASWA. Jukumu la kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa
kuwapata wanamichezo watakaowania tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila
mchezo.
Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na
TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha
michezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment