Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 19, 2016

VAN GAAL ASEMA YEYE BADO NI MENEJA WA MANCHESTER UNITED, MASHABIKI WANATEGEMEA MAKUBWA

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal amesema mategemeo miongoni mwa Mashabiki wa Timu hiyo ni makubwa mno baada ya Jana kumaliza Msimu wao wa BPL, Ligi Kuu England.
Jana Man United walifunga Msimu wao wakiwa kwao Old Trafford na kuifunga Bournemouth 3-1 kwa Bao za Wayne Rooney, Marcus Rashford na Ashley Young.
Mara baada ya Mechi hiyo kwisha Van Gaal aliingia kati ya Uwanja kuwahutubia Mashabiki na kuwashukuru kwa sapoti yao lakini Mashabiki hao wengi wao walimzomea.
Van Gaal, ambae Kikosi chake Jumamosi kinatinga Wembley Jijini London kuivaa Crystal Palace kwenye Fainali ya FA CUP, amekiri kuelewa kwanini amezomewa na kudai matarajio ya Mashabiki ni makubwa mno.
Van Gaal ameeleza: "Wanategemea makubwa. Lakini nadhani matarajio yao ni makubwa mno. Hii ni Timu ya mpito na hili nilisema tangu mwanzo!"
Msimu huu Man United wamepondwa sana kwa uchezaji wao hasa baada ya kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI Hatua ya Makundi na kisha kupelekwa EUROPA LIGI ambako nako walitolewa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Liverpool ambayo Leo inacheza Fainali ya Mashindano hayo na Sevilla.
Kwenye BPL, Man United wamemaliza Nafasi ya 5 ambayo inawapeleka moja kwa moja kuanza Hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI Msimu ujao.
Van Gaal ameeleza tatizo kubwa kwa Timu yake lilikuwa uhaba wa kufunga Magoli lakini kubwa zaidi lilikuwa Majeruhi yaliyowaandama hasa Miezi ya Novemba na Desemba.

Alimaliza: "Huwezi kuona Siku za usoni zikoje lakini unaweza kutathmini na kupima Siku zilizopita na hilo tutafanya ili tufikie maamuzi!"