Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 20, 2016

VAN GAAL ADAI KUTWAA KOMBE NI MUHIMU KULIKO KUCHEZA ULAYA

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal Leo amedai kwamba kutwaa FA CUP ni muhimu na mafanikio makubwa kupita kufuzu kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Jumamosi Man United watacheza Fainali ya FA CUP Uwanjani Wembley dhidi ya Crystal Palace wakiwania kulitwaa Kombe hilo kongwe Duniani kwa mara ya kwanza tangu 2004.

Hata hivyo, Wachambuzi huko England wamedai kutwaa FA CUP hakutapunguza presha ya kung’oka kwa Van Gaal hasa baada ya kushindwa kufuzu kucheza UCL Msimu ujao baada ya kumaliza Nafasi ya 4 kwenye BPL, Ligi Kuu England.
Wengi wa Wachambuzi hao wanaamini kuwa mara baada ya FA CUP Man United itamtimua Van Gaal aliebakisha Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na kumchukua Jose Mourinho.
Lakini mwenyewe Van Gaal anaona kubeba FA CUP ni muhimu kupita kucheza UCL kwani inaleta Kombe Klabuni.

Van Gaal ameeleza: “Kufuzu Ulaya si Taji…Taji ni FA CUP, ni Ubingwa. Ni muhimu kwa Wachezaji. Watabeba Kombe na kukumbuka hasa kwa hapa England kwani FA CUP ni Taji kubwa!”
Aliongeza: “Kwa Man United ni Taji kubwa. Nimesoma Klabu haijatwaa FA CUP tangu 2004!”
DONDOO MUHIMU:
-Hii ni Mechi ya Fainali ya 135 ya FA CUP.
-Fainali hii ni kama Marudio ya Fainali ya Mwaka 1990 ambayo Manchester United waliifunga Crystal Palace 1-0 baada ya Mechi ya kwanza kwisha Sare 3-3.
-Hii ni mara ya Pili kwa Palace kutinga Fainali wakati kwa Man United ni Fainali ya 18 na wameshinda 11 kati ya hizo wakipitwa tu na Arsenal walioshinda Fainali 12

-Mara ya mwisho kwa Man United kutwaa FA CUP ni Mwaka 2004 walipoifunga Timu ya Daraja la Kwanza Millwall 3-0.
Van Gaal atatinga kwenye Fainali hiyo akiwa na Kikosi kamili ukimwondoa Luke Shaw ambae bado hajawa fiti licha ya kuanza tena Mazoezi baada ya kuvunjika Mguu mara mbili Mwezi Septemba.
Pia Kungo Marouane Fellaini sasa yuko huru kucheza baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 3.


FA CUP
Fainali
Jumamosi Mei 21 

Saa 1:30 usiku
Uwanja wa Wembley, London

Manchester United v Crystal Palace