Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 25, 2016

MAN UNITED ILIMLIPIA NAULI VAN GAAL KURUDI KWAO URENO

Manchester United ilimlipia nauli ya ndege ya kibinafsi iliomsafirisha mkufunzi aliyefutwa kazi Louis van Gaal hadi nyumbani kwake huko Ureno siku ya Jumatatu.
Kupitia ombi lake,Man United ilikubali kuchelewesha thibitisho la kufutwa kwake hadi raia huyo mwenye umri wa miaka 64 alipokuwa safarini kuelekea Algarve na mkewe Truus.
Imebainika kwamba Man United ndio iliomlipia nauli hiyo.

United imekana kusema ni fedha ngapi ilizotumia ,lakini ndege ya kibinafsi kutoka Manchester hadi Ureno hugharimu pauni 10,000.

Van Gaal alifutwa kazi siku mbili baada ya kuisaidia Manchester United kushinda kombe la FA dhidi ya Crystal Palace.