Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 30, 2016

KINDA MARCUS RASHFORD AONGEZEWA MKWANJA KWENYE MKATABA NA MAN UNITED

KINDA wa Manchester United Marcus Rashford alieibuka Msimu huu na kuwa Staa amezawadiwa Mkataba mpya ulioboreshwa.
Straika huyo mwenye Miaka 18 alibakisha Mwaka Mmoja tu kwenye Mkataba wake wa sasa lakini sasa atapewa Mkataba wa muda mrefu na kuzoa Pauni 20,000 kwa Wiki.

Juzi, Rashford, akiichezea England kwa mara ya kwanza kabisa, alifunga Bao Sekunde 138 tu tangu Mpira wakati England inaichapa Australia 2-1 na kuweka Rekodi kuwa Kijana mdogo kabisa kuifungia England katika Mechi yake ya kwanza kabisa.

Rashford aliibuka Msimu huu kuchezea Man United alipochezeshwa kwa mara ya kwanza Timu ya kwanza dhidi ya FC Midtjylland kwenye Europa Ligi na kupiga Bao 2 na kisha tena kupiga Bao 2 walipocheza na Arsenal kwenye Ligi Kuu England.

Tangu wakati huo, katika Mechi 18 za Man United, Rashford amepiga Bao 8.
Mbali ya Rashford, Kijana mwingine wa Man United ambae nae amebakisha Mwaka mmoja na atapewa Mktaba mpya bora na mrefu ni Cameron Borthwick-Jackson.