Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 30, 2016

TERRY AMUUNGA MKONO JOSE MOURINHO

Kepteni wa Chelsea John Terry amemuunga mkono Jose Mourinho kufanikiwa kwenye Klabu yake mpya Manchester United huku akimueleza kuwa Meneja huyo ndie bora kupita yeyote aliewahi kucheza chini yake.
Terry alikaribia kuondoka Chelsea mwishoni mwa Msuimu huu baada ya Mkataba wake kumalizika lakini sasa ameongezewa Mwaka Mmoja na Msimu ujao atakuwa chini ya Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte ambae ni Meneja wa sasa wa Timu ya Taifa ya Italy.

Terry, ambae aliteuliwa na Mourinho kuwa Kepteni wa Chelsea wakati Mourinho alipotua Chelsea kwa mara ya kwanza Mwaka 2004, ameeleza: “Ni habari njema kwa Manchester United. Hii itawafurahisha Mashabiki na Wachezaji wa Man United kwani mara nyingi nimesema Mourinho ndie Meneja Bora niliewahi kufanya nae kazi!”