Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 22, 2016

MASHABIKI WA CASABLANCA WAUAWA

EDITORS NOTE: Graphic content / Moroccan youths lie on the pitch of the the Mohammed V stadium in Casablanca on March 19, 2016, following clashes between rival fans of Raja de Casablanca football club at the end of their match against Chabab Rif Al Hoceima. / AFP PHOTO / STRSTR/AFP/Getty Images


Mashabiki wawili wa kandanda walifariki dunia siku ya jumamosi baada ya mechi kali ya Raja de Casablanca ya Morocco na klabu ya Chabab Rif Al Hoceima.
Msemaji wa shirikisho la soka la nchi hiyo (FMRFF) amesema mashabiki walifokeana hata kabla ya mechi hiyo kuanza katika uwanja wa Mohammed wa Tano.
Hadi kufikia sasa haijajulikana kilichoibua uhasama huo miongoni mwa mashabiki wa Raja ambao walinaswa na kamera fiche wakivunja na kuharibu mali ya uwanja huo licha ya timu yao kuitandika Chabab Rif Al Hoceima mabao 2-1.
Utawala unasema kuwa watu zaidi ya 31 walikamatwa kufuatia machafuko hayo. Klabu ya Raja imepigwa faini ya diham laki moja sawa na pauni elfu saba. Vile vile Raja sasa italazimika kucheza mechi zake 5 zijazo pasi na mashabiki.