MCHECHETO wa mechi ya Ligi Kuu kati ya watani wa jadi
Simba na Yanga umeifanya Yanga kukodi ndege maalumu kwa ajili kwenda Mauritius
kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya awali
ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim.
Akizungumza na wandishi wa Habari jana, Mkuu wa Idara ya Habari
na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alisema wameamua kukodi ndege maalum ambapo
sasa wataondoka Ijumaa kwenda Mauritius badala ya jana kama ilivyoripotiwa
awali.
“Shirika la Ndege la Afrika Kusini limeshindwa kutupatia ndege ya kuunganisha
mapema mjini Johannesburg, kwenda Curepipe, Mauritius badala yake timu
ingelazimika kusubiri kwa saa saba na wakati wa kurudi badala ya kufika
Jumapili tungefika Jumatatu jambo ambalo lingefanya timu ikose siku tano za
kujiandaa na michezo mitatu ambayoinatukabili mmojawapo ni wa Simba,”alisema
Muro
Pia Muro alikiri kukodi ndege binafsi ni gharama lakini
wamelazimika kufanya hivyo ili kukwepa hujuma ambazo wameona dalili zake na
kumpa muda kocha kuendelea na programu yake kiufasaha na kuepuka uchvu kwa
wachezaji.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi saa 9:30 Alasiri katika Uwanja wa Curepipe na baada ya mchezo
huo timu itaondoka kurudi na itafikia kambini Kisiwani Pemba na Jumapili
itaanza mazoezi.
“Kocha ameendelea na programu yake leo na kesho (jana na
leo) na Ijumaa wataondoka na watafikia kwenye kambi maalum ambayo tumeandaa
ikiwa na wapishi wetu na baada ya mechi watapanda ndege kwani itakuwa
inawasubiri tayari kurudi na watafikia kambini Pemba,” alisema Muro
Muro amesema Yanga wanakabiliwa na mchezo dhidi yao na
Yanga, Mtibwa Sugar na Azam FC hivyo wanatakiwa kujiandaa vya kutosha kwani
michezo muhimu na ligi imekuwa na ushindani.
Wachezaji
Benedicto Tinocco ambaye ni kipa namba tatu na mshambuliaji Matheo Anthony na kiugo Godfrey
Mwashiuya wanakosa safari hiyo kutokana na sababu mbalimbali lakini Mwashiuya
hana pasi ya kusafiria.
Wachezaji waliokuwa majeruhi, Nahodha Nadir Haroub
‘Cannavaro’, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Amissi Tambwe wote
watasafiri na timu na mkuu wa msafara ni Ayoub Nyenzi, ambaye ni Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Kikosi kinachokwenda Mauritus ni Makipa;
Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deogratius Munishi ‘Dida’.
Mabeki ni Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou na Pato Ngonyani.
Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Issoufou Boubacar na Deus Kaseke.
Washambuliaji ni Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
Mabeki ni Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou na Pato Ngonyani.
Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Issoufou Boubacar na Deus Kaseke.
Washambuliaji ni Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
No comments:
Post a Comment