Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 6, 2016

WAYNE ROONEY NDIE BORA MWEZI JANUARI 2016

Wayne Rooney amechaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Manchester United kwa Mwezi Januari kwa Kura za Mashabiki wa Klabu hiyo.
Mwezi huo, Rooney, ambae ndie Nahodha wa Klabu hiyo, alitungua Bao 6 katika Mechi 6.
Katika upigaji Kura wa kuchagua Mchezaji Bora, Rooney alizoa Kura Asilimia 54 akifuatiwa na Anthony Martial na Cameron Borthwick-Jackson waliopata Kura Asilimia 36 na 10.
Rooney aliuanza Mwezi Januari kwa kufunga Bao la ushindi Man United walipocheza na Swansea City akiunganisha kwa kisigino pasi ya Anthony Martial.
Kisha akafunga Penati iliyowapa Man United ushindi wa 1-0 walipoitoa Sheffield United kwenye EMIRATES FA CUP na kufuata Bao zake 2 Man United walipotoka 3-3 na Newcastle huko Saint James Park.
Lakini Mashabiki wa Man United watalikumbuka sana Bao lake huko Anfield wakati Man United wanawafunga Mahasimu wao wakubwa Liverpool 1-0.
Rooney alifunga Mwezi Januari kwa Bao jingine wakati Man United inaipiga Derby County 3-1 kwenyy e EMIRATES FA CUP na kutinga Raundi ya 5.

Leo, huko Aon Training Complex, Kituo cha Mazoezi cha Man United Jijini Manchester, Rooney alikabidhiwa rasmi Kombe la kuashiria yeye ndie Bora kwa Januari.

No comments:

Post a Comment