Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 27, 2016

SIMBA KESHO KUCHEZA NA SINGIDA UNITED TAIFA KOMBE LA SHIRIKISHO
SIMBA kesho inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuivaa Singida United huku ikitamba kuwapa raha mashabiki wake na kufuzu hatua ya Robo Fainali Kombe la FA.

Kocha wa Simba, Jockson Mayanja amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi leo na kusahau matokeo ya kipigo cha mabao 2-0 walichokipata wiki iliyopita kutoka kwa Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja huohuo.

“Tumerekebisha makosa yetu na tumedhamiria kufanya vizuri, kila kitu kipo safi waje waone tunawapa raha,” alisema Mayanja.

Kauli kama hiyo ilizungumzwa pia na mshambuliaji Ibrahim Ajib, aliyesema hawataki kufanya makosa na wamejipanga kuwapa furaha mashabiki wao.

Mechi nyingine za michuano hiyo leo ni Panone FC watakuwa wenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi, huku Toto Africans wakicheza na Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Timu za Yanga, Ndanda FC na Coastal Union zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo.

Bingwa wa Kombe hilo, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (Caf) mwakani, huku Ligi Kuu Tanzania Bara bingwa wake akicheza Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.