Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 12, 2016

GEITA YAPEWA USHINDI BAADA YA JKT OLJORO KUGOMEA MECHI



TIMU ya Geita Gold imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya JKT Oljoro kugomea mchezo kati ya timu hizo uliochezwa Februari 6, kwenye Uwanja wa Nyankumbu Girls mkoani Geita.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema JKT Oljoro iligomea mechi hiyo dakika 70 baada ya kufungwa bao la pili kitendo ambacho ni kinyume cha Kanuni ya 29(1) ya Ligi Daraja la Kwanza.
“Kikao cha Kamati ya Kusimamia na kuendesha ligi maarufu kama kamati ya saa 72 ilikutana Jumatano na kupitia ripoti za waamuzi na makamishna wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la kwanza na kutoa maamuzi na mashauri mengine kupelewa kwenye kamati zingine za TFF,” alisema Wambura.
Pia imepigwa faini ya 1,000,000 kutokana na kitendo hicho kwa kuzingatia Kanuni ya 29(4), wakati wachezaji Shaibu Nayopa na Sunday Paul waliomvamia na kumpiga Refa wanapelekwa Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.
Naye Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro, Bunu Abdallah anapelekwa Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kumtolea lugha chafu mwamuzi msaidizi namba moja
Klabu ya Geita Gold imepigwa faini 1,000,000  na onyo kali kwa kukataa kuingia kwenye chumba cha wachezaji wakati wa mchezo wao na Polisi Tabora uliochezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Januari 31.
Polisi Tabora imepigwa faini ya 500,000 kutokana na kitendo cha mshabiki wake kupita pembezoni ya kwa kasi wakati mechi dhidi ya Geita Gold ikiendelea pia imepewa onyo kali kutokana kipa wa timu yake kuvaa jezi ambayo haikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Daraja la Kwanza wakati wa mechi hiyo.
Ligi daraja la kwanza inamalizika leo ambapo kundi A na kundi C zinatarajiwa kupata timu ambazo zitaungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

No comments:

Post a Comment