Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 2, 2016

Van Gaal: Man United 2015 ulikuwa mwaka wa mafanikio


article-2701780-1FE441FF00000578-425_634x407

Watu wengi wamekuwa wakiamini Manchester United kuwa mwaka 2015 ulikuwa mbaya kwao kwa kupata matokeo ambayo wengi hawajafurahishwa nayo lakini kocha wa klabu hiyo, Louis Van Gaal ameuzungumzia mwaka 2015 kama mwaka wenye mafanikio kwa kikosi chake kwa kufikia baadhi ya malengo ambayo walikuwa wamejiwekea.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao chake cha mwisho na vyombo vya habari kwa 2015, Van Gaal alisema katika msimu wa kwanza yeye kuingoza klabu hiyo walifikia malengo baadhi ambayo walitaka kuifikia mwaka huo.
Alisema katika msimu wa kwanza klabu hiyo ilifanikiwa kurudi katika timu nne za juu na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa licha ya kutolewa hatua ya makundi na hilo linadhihilisha ni jinsi gani klabu hiyo ilikuwa vizuri.
“Ulikuwa mwaka mzuri kwetu, tumefikia malengo kwa msimu wa kwanza ambao ulimalizika katikati ya mwaka 2015,
” Kwa msimu huu tulianza vizuri lakini mambo yakaanza kwenda tofauti tukatolewa Ligi ya Mabingwa jambo ambalo lilituumiza na bado tuna wakati mgumu lakini ukitoa mwezi Disemba mwaka 2015 tulikuwa vizuri,” alisema Van Gaal.
Aidha Van Gaal alizungumzia kama klabu hiyo ina nafasi ya kushinda kombe la Ligi Kuu ya Uingereza na kusema kama kikosi chake kikianza kupata matokeo mazuri  wanaweza kuwa na nafasi ya kutwaa kombe hilo.
“Kama timu ikicheza vizuri na kupata ushindi kwa mchezo ulio mbele yetu wa Swansea tunaweza kuwa na nafasi tumeshapoteza alama nyingi na tunatakiwa tushinde ili kuwasogelea,
” Matokeo mazuri ndiyo yanaweza kutufanya tushinde kombe lakini pamoja na hilo tunatakiwa kuongeza juhudi ili kumaliza katika nafasi za juu mwishoni kwa msimu na sio kumaliza katika nafasi za katikati”

No comments:

Post a Comment