Mchezaji
wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya LA
Galaxy ya nchini Marekani, Steven Gerrard amesema anapenda
kustaafu kucheza soka mwaka huu na kufanya kazi nyingine.
Gerrard
ambaye ambaye aliondoka Liverpool mwaka uliopita na kwenda kucheza
Ligi ya Marekani MLS ambayo kwa sasa imemalizika ameliambia gazeti la
Telegraph kuwa hana uhakika kwa asilimia zote kama utakuwa mwaka wake wa
mwisho lakini anapendelea iwe hivyo.
“Sina asilimia 100 lakini nafikiri utakuwa mwaka wangu wa mwisho wa kuwa kama mchezaji,” alisema Gerrard.
Baada
ya kuelezea mipango yake ya kutaka kustafu kucheza mpira mwaka huu,
Gerrard amezungumzia mipango yake baada ya kustaafu na kusema kuwa
anapendelea kuja kuwa kocha na huku akijilaumu kwa kutokutumia muda wake
vizuri aliokuwa nao na badala yake muda mwingi kuwa akitumikia katika
timu ya taifa ya Uingereza.
“Kiuhakika
naweza kuanza kupatikana mwezi Novemba au Disemba, 2016, kila mtu wa
soka duniani atajua kuwa kwa uhakika napatikana na nina matumaini 75%
nitakwenda katika mafunzo ya ukocha,
“Nilikataa
kuanza mafunzo ya ukocha nikiwa na miaka 21 au 22, muda wote nilipoteza
nikitumikia timu ya taifa katika hoteli kama mchezaji wa timu hiyo hata
nilipokuwa sina kazi ya kufanya nilikuwa naangalia tu ofisi na
kuangalia muziki wa bendi, natamani kama ningekuwa na CBA [leseni ya
ukocha] na sasa ningekuwa nafanya majaribio ya leseni yangu.
No comments:
Post a Comment