MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester United imekuwa ikifanya kimya kimya mchakato
kumrudisha Old Trafford straika wake wa zamani, Cristiano Ronaldo na kwa mujibu
wa taarifa zilizovuja karibuni, ni kwamba timu hiyo imepiga hatua kubwa sana.
Inasemekana Man United na Real Madrid wamekuwa kwenye
majadiliano kwa siku 12 sasa kujadili dau la pauni milioni 80 (Sh bilioni
192.483) – ambalo United wako tayari kulipa kwa ajili ya Ronaldo na mabingwa wa
Ligi Kuu England wana uhakika wa kumpata Mreno huyo.
David Moyes alilivalia njuga suala la Ronaldo wiki mbili
zilizopita, baada ya kupata taarifa kwamba Madrid wameongeza kasi kwenye mbio
zao za kumtaka Gareth Bale.
Na kwa mara ya kwanza, Real Madrid wako tayari kusikiliza
ofa ya United, baada ya Ronaldo mwenyewe kusema kwamba anataka kurudi England.
Mtendaji Mkuu mpya wa United, Ed Woodward, aliwasiliana na Rais
wa Madrid, Florentino Perez, huku akijua kwamba Ronaldo bado hajakubali
kuongeza mkataba mpya kwenye mkataba huu wa sasa ambao amebakiza miaka miwili.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Star, Perez alikuwa na
uhakika kwamba Ronaldo ataongeza mkataba wake wa sasa – na alishtuka baada ya
kugundua kwamba Mreno huyo anatamani kurudi Manchester United.
Hilo liliwafanya kukubali kuzungumza na United, kwa sababu
wanajua kwamba akibaki kwa msimu mwingine mwakani watamuuza kwa bei ya kutupa
mchezaji huyo waliyemlipia ada ya rekodi ya dunia mwaka 2009.
Hili linaeleza kwa nini Real Madrid wamepania kuvunja rekodi
ya dunia kumnasa staa wa Tottenham, Bale, katika harakati za kuwapoza mashabiki
baada ya Ronaldo kuondoka.
United wamekuwa hawafichi kuhusu nia yao ya kumnasa kiungo
wa Barcelona, Cesc Fabregas, kwa sababu wanataka watu watolee macho usajili huo
ili suala la Ronaldo liende kimya kimya bila kelele za vyombo vya habari.
Inasemekana sehemu ya mshahara wa Ronaldo italipwa na
kampuni ya magari ya General Motors (GM) ambayo imepanga kumfanya Ronaldo kuwa
balozi wao duniani kote.
Chevrolet, inayomilikiwa na GM, kuanzia msimu ujao itakuwa
mdhamini mkuu wa United na wanamuona Ronaldo kuwa mtu sahihi wa kutangaza
bidhaa zao, Amerika Kaskazini na Kusini wakati wa Kombe la Dunia mwakani.
Nike nao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mchakato mzima wa
kumnasa Ronaldo kwa sababu ni balozi wao muhimu.
Mpango wa kumsajili Ronaldo umefanya sakata la Wayne Rooney
kujiunga na Chelsea kusimama kwa muda.
No comments:
Post a Comment