Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 1, 2015

YANGA KUACHANA NA MBRAZIL COUTINHO


Kiungo Andrey Coutinho yuko jijini Dar es Salaam, lakini uongozi wa Yanga, umepitisha uamuzi wa kumtema. Uamuzi wa Yanga umepitishwa baada ya majadiliano kati ya uongozi na benchi la ufundi kukubaliana. Habari zinaeleza Yanga iko katika hatua za kufikia makubaliano na Coutinho ili kuvunja mkataba wake. Kocha Hans van der Pluijm ameridhia kuachana na Coutinho kwa kuwa amekuwa hana msaada wa kutosha. Lakini Yanga kwa sasa inafanya mchakato huo, kama pande mbili zitashindwa kufikia mwafaka, basi raia huyo wa Brazil ataendelea kubaki Yanga hadi mkataba wake utakapokwisha.