Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 1, 2015

WAGOMBEA FIFA Ballon d'Or TATU BORA, NI NEYMAR, MESSI, RONALDO

WAGOMBEA Watatu wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2015, FIFA Ballon d'Or, wametajwa Leo Jioni kutoka Listi ya Wachezaji 23 waliotangazwa Mwezi Oktoba na ni Mshika Tuzo hiyo Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar.
Ronaldo ndie Mshindi wa FIFA Ballon d'Or kwa Miaka Miwili mfululizo na kabla ya hapo Messi aliitwaa kwa mara 4 wakati Neymar ndio mara ya kwanza kuwemo humo.
Huu ni Mwaka wa 8 mfululizo kwa Ronaldo, anaechezea Real Madrid, na Messi, anaechezea Barcelona, kuwemo kwenye hii 3 Bora ya Wagombea wa FIFA Ballon d'Or.
Messi pia ni Mgombea kwenye Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka.


Kwa upande wa Wagombea wa Makocha Bora wapo Pep Guardiola wa Bayern Munich, Luis Enrique wa Barcelona na Jorge Sampaoli alieiongoza Chile kutwaa Copa America Mwezi Juni.
Kwa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Mchezaji wa USA, Carli Lloyd, Aya Miyama wa Japan na yule wa Germany Celia Sasic.

Sherehe ya kutunuku FIFA Ballon d'Or itafanyika Tarehe 11 Januari 11 2016 huko Zurich, Uswisi ambapo pia Makocha Bora, Mchezaji Bora kwa Kinamama na Mshindi wa Tuzo ya Puskas watatangazwa.