Baada ya kutajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia,
wanasoka walioingia kwenye Top 3 ya tuzo hiyo, Messi, Ronaldo na Neymar
usiku wa jana walipambana tena katika tuzo za La Liga.
Lionel Messi alitajwa kuwa mchezaji bora wa La Liga msimu uliopita mbele
ya Ronaldo katika tuzo hizo zilizofanyika huko Barcelona.
Baada ya kuiongoza Barca kushinda treble msimu uliopita, Luis Enrique nae akatajwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora.
Messi kwa mara nyingine tena akatajwa kuwa mshindi wa tuzo
mshambuliaji bora – hii ikiwa mara ya sita kushinda tuzo za uchezaji na
ushambuliaji bora wa La Liga.
Neymar
ambaye nae kwa mara ya kwanza ameingia kwenye top 3 ya Ballon D’or
alitajwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Amerika.
Golikipa
wa Barca, Claudio Bravo akashinda tuzo ya golikipa bora, huku kiungo wa
Valencia Sofiane Feghouli akishinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka
Afrika.
Cristiano
Ronaldo hakutoka kapa – akashinda tuzo ya mashabiki (5 Star Player
Award), huku Sergio Ramos akishinda tuzo ya beki bora na Tuzo ya kiungo
bora ikienda kwa James Rodriguez.
No comments:
Post a Comment