Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 22, 2015

VAN GAAL APEWA MECHI MBILI NA ED WOODWARD, AKIFUNGWA KUTIMULIWA

HUKU kukiwa na tetesi kuwa Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward amekuwa na Kikao mahsusi cha kujadili hatima ya Meneja wao Louis van Gaal kwenye Ofisi yao ndogo Jijini London na pia Sir Alex Ferguson kudaiwa kuombwa ushauri wa nini kifanyike, zipo habari nzito kuwa Klabu hiyo itafanya uamuzi mgumu muda si mrefu.
Zipo habari zinazodai kuwa Louis van Gaal atapewa Mechi 2 zijazo kurekebisha mwelekeo wa jahazi lakini zipo dalili pengine hata huo muda haupo.

Balaa kwa Louis van Gaal lilianza mara baada ya kuifunga Watford Bao 2-1 hapo Novemba 21 na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu England lakini tangu wakati huo hawajashinda hata Mechi 1 katika 6 walizocheza na kujikuta wakipigwa mara 3 mfululizo na pia kung’olewa kwenye 4 Bora ya Ligi.
MAN UNITED
Mechi zijazo za Ligi:
Desemba 26: Stoke City vs Man United
Desemba 28: Man United vs Chelsea
Januari 2: Man United vs Swansea City
Zipo tetesi kuwa hata Wachezaji wa Man United, hasa wale Maveterani, hawafurahishwi na uongozi wa Van Gaal huku Wachambuzi wengi wakidai Mdachi huyo sasa amepitwa na wakati na kinachomweka juu tu ni sifa zake alizozoa nyuma kwenye Historia yake.
Wapo wanaosema Van Gaal atang’oka na Msaidizi wake Ryan Giggs kupewa ukaimu hadi mwishoni mwa Msimu na Giggs akifanya vizuri katika kipindi cha ukaimu hapo ndipo atakuwa wa kudumu . 

Lakini pia zipo taarifa zinazodai Jose Mourinho, alietimuliwa na Chelsea Alhamisi iliyopita, ndie atashika wadhifa wa Umeneja wakati wowote kuanzia sasa.
Hadi sasa hamna mwenye uhakika nini kitajiri Man United na Klabu yenyewe haijazungumza chochote kama kawaida yao.
Wapo Wachambuzi wanaokumbushia jinsi David Moyes alivyotimuliwa Msimu wa 2013/14 ingawa dalili zilikuwepo kwa muda kwamba anaishi kwa Siku za kuhesabika lakini aliachwa kwenye wadhifa hadi Mwezi Aprili ilipofikia hatua kuwa Man United hawatafuzu tena 4 Bora na hivyo kutocheza UEFA CHAMPIONS LIGI na ndipo akafukuzwa.
Hadi sasa, kwa Man United, ndoto ya kumaliza ndani ya 4 Bora bado ipo hai lakini nani atakubali kila kukicha ni vipigo tu?

No comments:

Post a Comment