MENEJA
wa Arsenal Arsene Wenger amedai ushindi wao dhidi ya Man City ambayo ni
moja ya Timu inayotegemewa kutwaa Ubingwa wa England umewapa imani
kubwa ya kuwa Mabingwa.
Arsenal hawajatwaa Ubingwa tangu 2004 lakini Jana Uwanjani kwao Emirates Bao za Theo Walcott na Olivier Giroud za Kipindi cha Kwanza ziliwapa ushindi licha ya City kupata Bao mwishoni kupitia Yaya Toure na kutishia kuigeuza Gemu lakini Arsenal waligangamala na kushinda 2-1.
Baadae, Wenger, mwenye Miaka 66, alisema: "Ushindi umetufanya tujiamini, umetupa nguvu na imani."
Aliongeza: "Sasa Kikosi kimekomaa na hilo lilionekana wakati wa Gemu tulipokuwa kwenye presha."
Sasa Arsenal wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 4 mbele ya Man City walio Nafasi ya 3 na wako Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City.
Hii inamaanisha Arsenal wanakwenda Krismasi wakiwa Nafasi ya Pili na mara 5 kati ya 6 walizotwaa Ubingwa wa England kwa mara ya mwisho walitwaa Ubingwa wakiwa Nafasi ya Pili wakati wa Krismasi.
Mechi zijazo za Ligi kwa Arsenal:
Desemba 26 Southampton vs Arsenal
Desemba 28 Arsenal vs Bournemouth
Januari 2 Arsenal vs Newcastle

No comments:
Post a Comment