Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 3, 2015

GARY NEVILLE KOCHA MPYA VALENCIA

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Valencia ya Spain hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Neville, mwenye Miaka 40, ataendelea kuwa mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya England wakati akiendelea na wadhifa huu wake mpya huko Spain.
Uteuzi huu wa Neville umekuja kirahisi kwani Mmiliki wa Valencia, Peter Lim, Raia wa Singapore, pia ana Hisa kwenye Klabu ya huko Manchester, Salford City, ambayo pia Neville ni mmoja wa Wamiliki wake.
Ndugu wa Gary Neville, Phil Neville, aliteuliwa kuwa Kocha Msaidizi wa Valencia tangu Mwezi Julai.
Neville, ambae mara baada ya uteuzi huu wa huko Valencia amejitoa kuwa mmoja wa Wachambuzi wa TV ya Sky Sports, atatambulishwa rasmi Kesho Alhamisi na Rais wa Valencia Layhoon Chan.

Gary Neville-Maisha yake kwenye Soka:

1992: Alianza kuichezea Manchester United na kudumu Miaka 19 akitwaa Mataji makubwa 20 ikiwa ni pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI 2 na Ubingwa Ligi Kuu England mara 8.
1995: Alianza kuichezea England ambayo alikuja kucheza Mechi zake 85.
2011: Ajiunga na Sky Sports kama Mchambuzi.
2012: Ateuliwa kuwa Kocha Msaidizi wa England chini ya Roy Hodgson.
2014: Aliinunua Klabu ya Salford City pamoja na Wachezaji wenzake wa zamani wa Man United akiwemo Ndugu yake, Phil, Ryan Giggs na Paul Scholes.
2014: Wamuuzia 50% ya Salford City kwa Peter Lim, ambae ni Mmiliki mkuu wa Valencia


Jumamosi Valencia inacheza na Mabingwa Watetezi na Vinara wa La Liga, Barcelona, lakini Neville hataiongoza Timu na Mechi yake ya kwanza kwenye hatamu itakuwa ni Jumatano ya Wiki ijayo wakati Valencia inacheza Mechi ya Kundi lake la UEFA CHAMPIONS LIGI na Lyon.
Akiongelea hatua hii mpya, Kocha Mkuu wa England, Roy Hodgson, amesema uteuzi huu utainufaisha England kwa vile Neville atapata ujuzi zaidi wa Soka la Spain.
Huko Valencia, Neville anambadili Nuno Espirito Santo ambae alijiuzulu mara baada ya Jumapili Timu hiyo kufungwa 1-0 na Sevilla kwenye La Liga na kutupwa nafasi ya 9.
Msimu uliopita, Valencia ilimaliza Nafasi ya 4 lakini Msimu huu imedorora kwa kushinda Mechi 5 kati ya 13 za La Liga.