Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 31, 2015

JURGEN KLOPP NA BIG SAM WATOFAUTIANA

JANA Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ilibidi atulizwe munkari na Polisi ya kumpandishia Meneja mwenzake wa Sunderland Sam Allardyce wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stadium of Light.
Klopp alipandwa na jazba wakati Jeremiah Lens wa Sunderland alipomchezea rafu mbaya Beki wa Liverpool Mamadou Sakho.
Wakati huo Liverpool walikuwa tayari washafunga Bao lao pekee na la ushindi kupitia Christian Benteke aliefunga Dakika ya 53.
Klopp aliamini Sakho ameumia vibaya na Lens alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu lakini Refa alimpa Kadi ya Njano.
Hapo ndipo Klopp alipoanza kumbatukia Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, na munkari ulipopanda Polisi waliingia kati kumtuliza Klopp.
Baadae, Allardyce alisema Klopp alitumia maneno mabovu na ya matusi na kumweleza Meneja huyo wa Liverpool kama 'Mjerumani laini'.
Hata hivyo, bifu halikuendelea kwani mwishoni Mameneja hao walipeana mikono kama ilivyo desturi Mechi ikimalizika.