Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 19, 2015

JOSE MOURINHO KUENDELEA NA SOKA LONDON LAKINI ATAKA FARAGHA IHESHIMIWE

José Mourinho amesema hatachukua Likizo ili kupumzika baada ya kutimuliwa Chelsea hivi Juzi bali atabaki Jijini London na kutua Viwanjani kusaidia Marafiki zake.
Mawakala wa Mourinho wamesema hayo kupitia Taarifa maalum ambayo pia iliwashukuru Mashabiki wa Chelsea kwa sapoti yao.
Taarifa hiyo ilikiri kuwa mara zote alikuwa ni Mourinho alieamua kuaachana na Klabu lakini safari hii, kwa mara ya kwanza, ni Chelsea ndio ilimtema Juzi Alhamisi.
Mourinho pia amesema anasikia fahari kubwa kwa kuiwezesha Chelsea kutwaa Makombe 8 katika vipindi vyake Viwili na Klabu hiyo.
Pia alisistiza kuwa hatapumzika kwa vile hasikii uchovu na hivyo anasubiri kwa hamu nini kitajiri kwake hivi karibuni.
Kwa sababu anaipenda Soka, Mourinho atatua Viwanjani ili kufanya kazi na kuwasapoti Marafiki zake lakini hatahudhuria Mechi kubwa ili kutoanzisha uvumi wowote kuhusu yeye.
Mourinho amesema atabaki Jijini London lakini ameomba faragha yake na ya Familia yake iheshimiwe huku akisisitiza kuwa hataongea lolote kuhusu hali yake ya sasa na kuwataka Wanahabari waheshimu hilo.