Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 3, 2015

DIVOCK ORIGI AKIPIGA HAT-TRICK LIVERPOOL IKISHINDA MABAO 6-1 DHIDI YA SOUTHAPTON KWENYE CAPITAL ONE CUP

Bao za Liverpool leo hii zimefungwa na
Daniel Sturridge 25'
• Daniel Sturridge 29'
• Divock Origi 45'
• Divock Origi 68'
• Jordon Ibe 73
• Divock Origi 86' Mane akishangilia bao lake la pekee kwa Southampton1-0 bao lilifungwa dakika ya kwanza tuu
Furaha kwa Klopp
Southampton bao lao likifungwa mapema dakika ya kwanza na
Sadio Mane 1' 
Liverpool iliicharaza Southampton Bao 6-1 kwenye Mechi ya mwisho ya Robo Fainali ya C1C, Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi huko England, na kutinga Nusu Fainali.Katika Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Mtakatifu Maria, Southampton walitangulia kufunga Dakika ya Kwanza tu kwa Bao la Sadio Mane lakini Liverpool wakajibu kwa Bao 2 za Daniel Sturridge, ambae alianza Mechi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu wa Majeruhi, katika Dakika za 25 na 29, na Bao la 3 kufungwa na Divock Origi katika Dakika ya 45.Kipindi cha Pili, Origi alikamilisha Hetitriki yake katika Dakika za 68 na 86 na Dakika ya 76 Ibe alifunga Bao moja.
Mara baada ya Mechi hiyo kumalizika, ilifanyika Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali na Manchester City kupangwa na Everton wakati Liverpool watacheza na Stoke.
Mechi za Nusu Fainali huchezwa kwa mikondo miwili, ya Nyumbani na Ugenini, na Everton wataikaribisha Man City Goodison Park katika Mechi ya kwanza wakati Stoke watakuwa Nyumbani Britannia Stadium kuivaa Liverpool.
Mechi za Kwanza zitachezwa hapo Januari 5 na 6 na Marudiano ni Januari 26 na 27. 
3-1Ibe akifunga bao la tanoFull kushangilia

CAPITAL ONE CUP: DROO YA NUSU FAINALI: 
Mechi kuchezwa Januari 5 na 6 
Everton v Man City [Goodison Park] 
Stoke City v Liverpool [Britannia Stadium]

Marudiano 
Mechi kuchezwa Januari 26 na 27
-Man City v Everton [Etihad]
-Liverpool v Stoke City [Anfield]

Capital One Cup
Robo Fainali
Matokeo:
Jumanne Desemba 1

Middlesbrough 0 vs Everton 2
Stoke City 2 vs Sheffield Wednesday 0
Manchester City 4 vs Hull City 1