Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 27, 2015

Rose Muhando aahidi makubwa, Shusho ndani Krismas Dar


Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la Krismasi la kumshukuru mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambao ni waandaaji wa tamasha hilo.
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Rose Muhando, ameanza kujifua kwa ajili ya kufanya kweli katika Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25 katika Ukumbi wa Diambond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Muhando mmoja wa waimbaji waliothibitishwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa lengo la kuwaleta pamoja wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili kufurahia tukio la kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo, alisema ataimba vibao vyake vya zamani na nyimbo mpya. “Namshukuru Mungu kunijalia kipaji na karama ya uimbaji, pia kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa washiriki wa Tamasha la Krismas. Kwa upande wangu ni fursa muhimu kuzidi kumtukiza Mungu kwa sauti aliyonijalia,” alisema Muhando na kuongeza:

“Nimejiandaa vizuri kwani wakati wowote mimi nimekuwa nikijiweka hali ya utayari katika kumtumikia
Mungu kwa kipaji hiki cha uimbaji.
“Nawalika wapenzi wa nyimbo za injili na wapendwa wote, waje Diamond Jubilee tufurahie Krismas na tuseme asante Mungu kuivusha salama nchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,” alisisitiza.
Alisema, kwa kushirikiana na waimbaji wengine wa ndani na nje ya nchi, watajitahidi kulitendea haki Tamasha hilo akiamini ni tumkio la kimataifa hivyo hata maandalizi yake yanapaswa kubeba uzito huo na siyo vinginevyo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama, amemtaja Christina Shusho kushiriki Tamasha hilo akiungana na wengine huku waimbaji wengine wataendelea kujulikana baada ya kukamilika kwa mazungumzo na waratibu.
Shusho, mwimbaji aliyewahi kutamba na vibao mbalimbali kama Unikumbuke na vinginevyo, yu miongoni mwa waimbaji waliowajaaliwa kipaji cha kumtumikia Mungu kwa njia hiyo ya uimbaji kwani ujumbe wa nyimbo zake umekuwa ukiwabariki, kuwajenga wengi kiimani na kuacha matendo mabaya.