Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 27, 2015

BAADA YA SARE YA 0-0, VAN GAAL ASEMA WAKO TAYARI KWA WOLFSBURG DESEMBA 9

BAADA Jana kushindwa kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, walipotoka 0-0 na PSV Eindhoven Uwanjani OldcTrafford, Manchester United sasa wana kibarua kigumu katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B Ugenini na VfL Wolfsburg hapo Desemba 8.
Jana Wolfsburg waliitwanga CSKA Moscow 2-0 na kukaa kileleni mwa Kundi B wakiwa na Pointi 9 wakifuatiwa na Man United wenye Pointi 8 na PSV Pointi 7.
Timu 2 za juu kwenye Kundi husonga Raundi ya Mtoano na ya 3 kutupwa EUROPA LIGI.
Katika Mechi ya mwisho, Wolfsburg, wakiwa Nyumbani, wanahitaji Sare tu kufuzu matokeo ambayo yatawatupa nje Man United ikiwa PSV, wakicheza kwao, itaifunga CSKA ambayo ishaaga mashindano.

Ili kufuzu, bila kujali matokeo mengine, Man United inabidi iwafunge Wolfsburg huko huko kwao Ujerumani.
Mara baada ya Mechi ya Jana waliyotawala na kukosa Bao kadhaa, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, alisema: "Lolote linaweza kutokea, Sisi tuna uwezo kushinda popote! Tumeonyesha hilo kwenye Ligi Kuu England sasa na lazima tufanye hivyo kwenye UCL. Tutaenda Wolfsburg na matumaini!"
Wakati Man United ni wagumu kufungika, hasa Nyumbani ambako hawajafungwa Bao lolote katika Mechi 5 zilizopita, wao kufunga imekuwa taabu kwani wamefunga Bao 6 tu katika Mechi zao 8 zilizopita.
Hilo limemfanya Kepteni wao Wayne Rooney akiri wapo butu na inabidi wawe 'makatili'.
Matumaini kwa Man United ni kuwa mwishoni mwa Septemba Man United iliifunga Wolfsburg, ambayo ipo Nafasi ya 3 kwenye Bundesliga, Bao 2-1 Uwanjani Old Trafford kwa Bao za Juan Mata na Chris Smalling.
Van Gaal anesisitiza: "Tuliwafunga Nyumbani, kwa nini tusishinde Ugenini? Bado tupo Nafasi ya Pili na ni nafasi ya kufuzu