Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 27, 2015

BARCELONA WAANDAA KUMPA MKATABA MPYA NEYMAR

FC Barcelona na Neymar zinakaribia kusaini Mkataba mpya ambao utamfanya Kepteni huyo wa Brazil kuzoa Euro Milioni 15 kwa Msimu.
Donge hilo nono litamfanya awe Mchezaji wa 3 Duniani anaelipwa Mshahara wa juu kabisa akiwa nyuma ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Hivi sasa Neymar inasemekana analipwa Euro Milioni 8.8 kwa Mwaka.
Habari hizi zimetobolewa na Jarida la Marca huko Spain ambalo limesema Mkataba huo mpya utaongeza juu Dau lake ikiwa Klabu nyingine itataka kumnunua ndani ya Mkataba kutoka Euro Milioni 180 za sasa na kufikia Euro Bilioni 1 ingawa Wawakilishi wa Neymar wanataka Kipengele hicho kigote kwenye Euro Milioni 250.

Mkataba huo mpya utamweka Neymar, mwenye Miaka 23, Klabuni Barca hadi Juni 2021.

Hivi karibuni kulikuwa na minong’ono kuwa Neymar ataondoka Barca kutokana na kuwepo Kesi inayohusisha Uhamisho wake kutoka Klabu ya Brazil Santos kwenda Barca ambayo Baba yake Mzazi Neymar nae amehusishwa kwenye njama zinazodaiwa Barca ilifanya ili kukwepa kulipa Kodi huko Spain kwa kuficha gharama halisi za Uhamisho huo.

Hivi sasa Neymar anang’ara mno kiasi ambacho Wachambuzi wanatambua muda si mrefu atatwaa Ballon D'Or hasa ukizingatia umri wake ni mdogo ukilinganisha na Messi na Ronaldo ambao sasa wanaanza ‘kuzeeka’ Kisoka.