DC
Makonda akitoa hutuba ya uzinduzi.
|
Mwanzilishi
wa umoja huo, Stellah Rwabutaza (kushoto), akimlisha keki mgeni rasmi DC
Makonda. Katikati ni mdau wa Keki Cynthia Henjewele.
|
Muakaji
keki, Roselins Sia Adhero (kulia), akimkabidhi keki DC Makonda.
|
Uongozi wa TCBA wakiwa kwenye picha ya pamoja |
Waokaji keki wakifurahia jambo |
Na Rahel
Pallangyo
MKUU wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewataka waokaji keki kufanya kazi yao kwa
kushirikiana kwani inasaidia kuinua uchumi wa nchi.
Makonda aliyasema
hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua Chama cha Waokaji keki Tanzania (TCBA)
katika hafla iliyofanyika ukumbi wa City Lounge Posta mpya ambapo alikuwa mgeni
rasmi.
"Kazi
mnayoifanya inalisaidia taifa kuinua uchumi kwani inatoa ajira kwa wengine kikubwa
endeleeni kuwa wabunifu zaidi wa kutengeneza keki za aina mbalimbali"
alisema Makonda.
Makonda
aliwataka waokaji keki hao kila mmoja wao kujisogeza zaidi kwa kupanua wigo wa
kazi zao kwa kuwa na vyombo vya muziki, kupiga picha za manato na video badala
ya kila kazi kufanywa na mtu mwingine.
Pia
aliwaambia wajiandae kwani ofisi yake imeandaa Sh.20,000,000 kwa ajili ya kushindanisha
wazo bora la andiko la biashara na kuwataka nao waingie kujaribu bahati yao.
Mwanzilishi
wa umoja huo, Stellah Rwabutaza alisema amesaidia kuwaunganisha waokaji keki
nchini na wameweza kutambuana na kubadilishana ujuzi.
"Kwakweli
umoja huu umetuunganisha sisi waokaji wa keki jambo litakalosaidia kufanya kazi
zetu kwa pamoja" alisema Stellah.
Stellah
alisema changamoto kubwa waliyonayo ni kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa
Tanzania (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwakamata mara kwa
mara ambapo waliomba watoe maelekezo ya nini wafanye ili kuendeleza kazi yao
hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa TCBA, Philip Mbonde,
alisema umoja huo umewafanya wawe na mtandao wa kutafuta masoko ya keki na
kujifunza ubunifu wa kutengeneza keki za aina mbalimbali.
No comments:
Post a Comment