Kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo, Argentina wamebakia Namba 1 huku Mabingwa wa Dunia Germany wakipanda na kukamata Nafasi ya Pili wakati Tanzania imebaki pale pale Nafasi ya 140.
Kwenye 10 Bora, Belgium imeshuka na kushika Nafasi ya Tatu, Portugal wamepanda hadi Nafasi ya 4 na Spain kurudi 10 Bora baada ya Miezi Mitatu na sasa wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 5.
Kwa Afrika, Timu ya juu bado ni Ivory Coast na imebakia nafasi yake ile ile ya 21 ikifuatiwa na Ghana walio Nafasi ya 25.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa Tarehe 5 Novemba 2015.
10 BORA:
1 Argentina
2 Germany
3 Belgium
4 Portugal
5 Colombia
6 Spain
7 Brazil
8 Wales
9 Chile
10 England
No comments:
Post a Comment