Nathaniel Kerr, 24, alikiri mashtaka mbele ya hakimu katika mahakama mjini Manchester, Uingereza.
Mchezaji aliyeumizwa Stuart Parsons, 30, alikuwa akijibizana na mmoja wa mchezaji mwenzake Kerr kwenye mechi ya ligi ya Sunday muda mfupi kabla ya kisa hicho uwanjani katika eneo la Stockport.
Kerr alimkanyaga Parsons mara kadha hadi mguu wake ukavunjika na ilimbidi kufanyiwa upasuaji na kukaa wiki kadha hospitalini.
Parsons alipokuwa amelala uwanjani akiwa na maumivu tele, Kerr alimwambia mwenzake kwa sauti: “Nimefanya haya kwa ajili yako”
Konstebo wa polisi Louise Spencer, wa kikosi cha polisi cha eneo kubwa la Mancheste, alisema: "Jeraha hili lilimwathiri sana mwathiriwa, na hakuweza kufanya kazi wala kusaidia familia yake change.
"Alilazimika kutegemea hisani ya wachezaji wenzake waliolazimika kufanya michango kukidhi mahitaji yake ya kifedha.
"Wakati huo wote, Kerr hajaonyesha majuto yoyote.”
Alisema kukamatwa na kuadhibiwa kwa Kerr ni ishara kwamba “uhuni na ujambazi” katika mechi za kandanda hautavumiliwa tena.
No comments:
Post a Comment