Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 2, 2015

HODGSON ATANGAZA KIKOSI CHA ENGLAND CHA MECHI ZA EURO 2016, DELE ALLI NDANI

KOCHA wa England, Roy Hodgson, ametangaza Kikosi chake kwa ajili ya Mechi zao za mwisho za Kundi E la EURO 2016 ambalo wao tayari wamefuzu kwenda Fainali huko France Mwakani huku wakiwa na Mechi kadhaa mkononi.
Lakini, Hodgson hakumchukua Straika wa Liverpool Daniel Sturridge ambae alikuwa nje kitambo akiwa majeruhi na kurejea Uwanjani hivi Juzi tu.
Wachezaji ambao wamerejeshwa Kikosini baada ya kuachwa ni Beki wa Southampton Ryan Bertrand, Beki wa Manchester United Phil Jones na Kiungo wa Liverpool Adam Lallana.
England watacheza na Estonia Uwanjani Wembley Jijini London hapo Oktoba 9 na kisha Ugenini na Lithuania hapo Oktoba 12.
KIKOSI KAMILI:
Makipa:

Jack Butland (Stoke City), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley)

Mabeki:
Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton)
Viungo:
Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jonjo Shelvey (Swansea City), Raheem Sterling (Manchester City)

Mafowadi:
Danny Ings (Liverpool), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Wayne Rooney (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester City), Theo Walcott (Arsenal)

No comments:

Post a Comment