Kwa
mujibu wa Jarida linaloheshimika Duniani kwa mambo ya Kifedha, Forbes,
Staa wa Barcelona, Lionel Messi, hayumo kwenye 10 Bora ya Dunia kwa
Wanamichezo wenye thamani za juu Duniani huku kwenye 10 Bora ya Timu,
zipo Klabu 3 tu za Soka miongoni mwake.
Mwaka 2014, Messi alikuwemo kwenye 10 Bora ya Wanamichezo akishikilia Nafasi ya 9 lakini Mwaka huu hayumo kabisa. Mchezaji Bora wa Soka Duniani, Cristiano Ronaldo, yeye yupo kwenye 10 Bora akikamata Nafasi ya 8 wakati Mwaka Jana alikuwa Nafasi ya 7.
Kwenye 10 Bora ya Wanamichezo, Nambari Wani ni Tiger Woods mwenye thamani ya Dola Milioni 30.
Kwa upande wa 10 Bora ya Timu, Timu yenye thamani ya juu kabisa ni New York Yankees na Klabu za Soka ambazo zimo humo ni Real Madrid iliyo Nafasi ya 5 huku Nafasi za 6 hadi 8 ni Manchester United, Barcelona na Bayern Munich.
FORBES-Listi za Ubora-Thamani za Juu:
10 BORA-Wachezaji wa thamani ya juu:
1. Tiger Woods - Worth $30m
2. Phil Mickelson - $28m
3. LeBron James - $27m
4. Roger Federer - $27m
5. MS Dhoni - $21m
6. Usain Bolt - $18m
7. Kevin Durant - $18m
8. Cristiano Ronaldo - $16m
9. Rory McIlroy - $12m
10. Floyd Mayweather Jr - $11.5m
10 BORA-Timu za thamani ya juu:
1. New York Yankees - $661m
2. Los Angeles Lakers - $521m
3. Dallas Cowboys - $497m
4. New England Patriots - $465m
5. Real Madrid - $464m
6. Manchester United - $446m
7. Barcelona - $437m
8. Bayern Munich - $375m
9. Los Angeles Dodgers - $373m
10. New York Knicks - $361m
No comments:
Post a Comment