Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 6, 2015

KESI YA HASANOO: SHAHIDI ASEMA KONTENA HALIKUKAGULIWA



SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kusafirisha Meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 1.2,  inayomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Simba, Hassan Othuman ‘Hassanoo’ na wenzake ameieleza mahakama kuwa kontena lililosafirisha meno hayo lilipita bandarini bila kukaguliwa.
Aidha alidai hati za kusafirisha kontena hilo lenye namba BISU 2334468 na serial namba 243899 zilionyesha linasafirisha mifuko 381 ya mbegu za alizeti yenye kilo 12,000 kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Hong Kong nchini China.
Ofisa upelelezi, Meja Chuchi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam, alidai kuwa Kontena hilo lilipewa kibali cha kuingia bandarini na Ofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Lusekelo Mwakajiga ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo, bila kukaguliwa kwakuwa awali ilidaiwa kontena hilo bado halijawasili Dar es Salaam likitokea Arusha.
Akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali Lilian Itemba, Meja Chuchi alidai Novemba 19, 2012, akiwa ofisini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Msangi alimwambia aende makao makuu ya polisi, huko alikutana na askari wengine pamoja na maofisa wa Idara ya wanyamapoli kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Alidai, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Herry aliwaambia Jeshi la polisi kupitia Kitengo cha polisi wa kuimataifa (Interpol) wamepata taarifa kwa njia ya barua pepe  kutoka kitengo cha Interpol HongKong China, kuhusu kukamatwa kwa kontena likiwa na vipande vya meno ya tembo lililotoka bandari ya Dar es salaam.
Chuchi alidai kuwa, katika upelelezi wa awali walibaini kuwa Wakala aliyetumikakusafirisha mzigo huo ni Mjemwa Crealing & Fowarding Company Ltd inayomilikiwa na mshitakiwa Ally Kimwaga akishirikiana na mwenzake Ramadhani Pazi ambaye bado hajakamatwa na anatafutwa na Polisi.
Alidai Kimwaga alipokamatwa alikutwa na hati za kusafirishia kontena hilo, aidha alidai mzigo huo ulikuwa wa Hassanol pia mzigo ulipakiwa katika yadi iitwayo Rofal General Trading Co.Ltd iliypopo eneo la kurasini na ulitolewa katika yadi hiyo na gari lenye namba T 888 AKL kwenda bandarini.
Meja Chuchi aliongeza kuwa, dereva wa gari hilo Iddy Mohamed, aliwapeleka kwenye yadi hiyo  inayodaiwa kumilikiwa na ndugu wa Hassanoo aliyetajwa kwa jina la Abdalah na walipofanya ukaguzi walikuta mabaki ya mbegu za alizeti, magari matatu yenye anuani ya mshitakiwa Hassanoo na kwamba yadi hiyo inajihusisha na uhifadhi wa vyuma chakavu.

No comments:

Post a Comment