Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi
elfu saba (7,000).
Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni shilingi Elfu
Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti
vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa
ni kwa viti vyenye rangi ya Bluu, Kijani na Orange.
Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili
asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni –
Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry
– Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya
mabasi ya daladala.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchin
kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili
kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA,
Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand
Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa
mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya Jumamosi itakua
ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons)
watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya.
Maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Stand United katika uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar
watawakaribisha Majimjaji ya Songea katika uwanja wa Manungu wakati
Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili ambapo waoka
mikate wa Azam FC watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa Chamazi
Complex, huku African Sports wakiwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment