Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Bado tunaendelea kutazama rekodi
mbalimbali zilizopita baina ya klabu za Simba na Yanga klabu hizi
hasimu Tanzania zitavaana tena Jumamosi hii katika mchezo wa raundi ya
nne wa ligi kuu bara.
Kuelekea mchezo huo, Yanga haijapata ushindi dhidi
ya Simba tangu Mei, 2013 waliposhinda 2-0. Hiyo inamaanisha kwamba
mabingwa hao mara nyingi zaidi bara wataingia uwanjani kusaka ushindi
wao wa kwanza ndani ya miaka miwili.
Je, unajua ya kwamba Simba
imewahi kucheza gemu 15 mfululizo za ligi kuu dhidi ya Yanga pasipo
kupoteza?. Kati ya Septemba 1, 2001 hadi April 27, 2008 Simba ilikuwa
haijui suala la kupoteza mchezo wa Dar es Salaam Derby.
CHEKI MATOKEO YA GEMU 15 MFULULIZO AMBAZO SIMBA HAIKUPOTEZA DHIDI YA YANGA KATIKA LIGI KUU BARA PEKEE
Septemba 1, 2001, Simba 1-0 Yanga
Goli pekee la mshambulizi
aliyekuwa na misuli na uwezo wa kupiga mashuti makali, Joseph Kaniki
’Golota’ katika dakika ya 76 lilisimama hadi mwisho. Yanga ilipoteza
mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru. Ikumbukwe kabla ya timu hizo
kuvaana mara mbili mwaka 2000. Simba walishinda 2-1 katika mchezo wa
mzunguko wa kwanza April 23. Yanga wakashinda 2-0 katika gemu ya
marejeano Agosti 5.
Septemba 30, 2001. Yanga 1-1
Joseph Kaniki alifunga goli lake
la pili katika Dar es Salaam Derby dakika ya 65′. Zikiwa zimesalia
dakika 4 gemu kumalizika, Sekilojo Chambua akaisawazishia Yanga na
kutengeneza sare ya kufungana 1-1.
Agosti 18,2002, Simba 1-1 Yanga
Dakika ya 65′ iliendelea kuwa
mbaya kwa Yanga kwani safari hii, Madaraka Suleimani ‘ Mzee wa Kiminyio’
alifunga goli la kuongoza upande wa Simba lakini kwa mara nyingine,
Sekilojo Chambua akaisawazishia timu yake dakika moja kabla ya
kumalizika kwa mchezo na kutengeneza matokeo ya 1-1.
Novemba 10, 2002, Yanga 0-0 Simba
Ilikuwa sare ya tatu mfululizo
katika ligi kuu na mechi ya kwanza isiyo na magoli katika karne
mpya.Septemba 28, 2003, Simba 2-2 Yanga.
Ilikuwa moja ya mechi za kuvutia
mwanzoni mwa miaka ya 2000. Simba ilikuwa mbele kwa magoli 2-0 kufikia
dakika ya 36 kupitia kwa mshambulizi wake, Emmanuel Gabriel dakika za
27′ na 36′.
Kiungo mshambuliaji, Kudra Omari
akapunguza presha kwa wapenzi wa timu yake baada ya kufunga zikiwa
zimesalia dakika 3 mchezo kwenda mapumziko. Mshambulizi, Hernry Morris
akaisawazisha Yanga dakika ya 55′ na hadi mwisho wa mchezo matokeo
yalikuwa 2-2.
Novemba 2, 2003, Yanga 0-0 Simba.
Ilikuwa mechi mbaya licha ya
Simba kuwa na msimu mzuri katika michuano ya kimataifa. Ilikuwa sare ya
tano mfululizo huku ukiwa mchezo wa sita mfululizo Yanga wanashindwa
kupata ushindi. Mechi ilimalizika kwa suluhu-tasa.
Agosti 7, 2004, Simba 2-1 Yanga
Mshambulizi raia wa DR Congo,
Pitchou Kongo alifunga goli la kuongoza upande wa timu yake dakika ya
48′. Yanga iliongoza mchezo wa Dar es Salaam derby kwa mara ya kwanza
tangu April 23, 2000 lakini wakajikuta wakipoteza tena mchezo. Idd Moshi
alifunga dakika ya 4′ lakini, Steven Mapunda ‘ Garrincha’ akafunga mara
mbili dakika za 59′ na 72′ na kuisaidia Simba kushinda 2-1 msimu wa
mwaka 2000.
Baada ya Pitchou kufunga Simba
walitulia na kufuga Simba wakapata magoli mawili ya ‘ chap chap’ kupitia
kwa kiungo, Shaaban Kisiga dakika ya 64′ na Ulimboka Mwakingwe dakika
ya 76′ na kushinda mechi.
Septemba 18, 2004, Yanga 0-1 Simba
Moja ya magoli maridadi ambayo
yatakumbukwa sana katika mipambano ya Simba na Yanga ni lile
lililofungwa na Athumani Machuppa dakika ya 84′ akiwa amepokea pasi na
Suleimani Matola ambaye alikimbia haraka na mpira kutoka katika eneo lao
la kujilinda, Matola ‘ alipunguza’ uwanja, Machuppa alikuwa amebaki
mbele peke yake na walinzi, Samson Mwamanda na Salum Athuman (kama
kumbukumbuka ziko sawa).
Kilichokuja kutokea ni goli kali.
Alikimbilia pasi ya Matola na huku akikokota mpira kwa kasi akitoke
wing ya kushoto, Machuppa alimpiga chenga ya hatari Mwamanda ambaye
aliteleza na kubaki akimtazama Machuppa akipeleka mpira katika ‘angle’
na kuimaliza mechi. Baada ya mechi hiyo mahusiano ya Mwamanda na Yanga
yakaingia doa na pengine alivuliwa thamani yake yote kiuchezaji .
April 17, 2005, Simba 2-1 Yanga
Katika uwanja wa Jamhuri,
Morogoro, Simba ikiwa chini ya kocha wa muda, Jamhuri Kihwelo ‘ Julio’
sambamba na Boniface Pawassa katika benchi ilishinda 2-1. Yanga
walitangulia kuongoza kupitia kwa kiungo Aaron Nyanda dakika ya 39′
lakini mshambulizi aliyekuwa na umbo kubwa, Nurdin Msiga akasawazisha
dakika moja kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza. Athumani
Machuppa akazamisha goli la pili dakika ya 64′.
Agosti 21, 2005, Yanga 0-2
Simba. Ilikuwa gemu ya mwisho ya
Dar es Salaam derby kwa nahodha-mshindi, Matola na kiungo mshambulizi,
Nico Nyagawa akatupia kambani mara mbili katika dakika za 22′ na 56′
katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, Arusha na kuipa Simba ushindi wa
2-0. Baada ya mechi hiyo Matola aliruhusiwa kujiunga na Super Sport
United ya Afrika Kusini.
Machi 26, 2006, Simba 0-0 Yanga
Baada ya kupoteza mechi nne mfululizo Yanga walilazimisha suluhu-tasa katika gemu ya kwanza msimu wa 2006.
Oktoba 29, 2006, Yanga 0-0 Simba
Mechi hii ya marejeano ilimalizika kwa suluhu-tasa pia hivyo kutengeneza matokeo ya kutofunga katika michezo yo.
FAINALI LIGI KUU NDOGO, Jula 8, 2007, Simba 1 ( 5)-1 ( 4) Yanga
Shirikisho la mpira wa miguu
nchini, TFF liliamua kurekebisha kalenda yake ya mashindano na hapo
wakahitaji kuachana na mfumo wa zamani wa uendeshaji wa ligi kuu kutoka
Machi-Septemba na kuwa, Agosti -Mei, ili kuendana na kalenda za
kimataifa, hivyo ili kupata wawakilishi wa nchi katika michuano ya
kimataifa timu za ligi kuu zikapangwa katika makundi, kisha hatua ya
nusu fainali na fainali ikawakutanisha mahasimu Simba na Yanga katika
uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mshambulizi, Mkenya, Moses
Odhiambo akaifungia Simba goli la kuongoza kwa mkwaju wa penalti dakika
ya 2′ tu ya mchezo lakini, kiungo mshambulizi, Said Maulid ‘ SMG’
akaisawazisha Yanga dakika ya 55′ na mechi ikamuuliwa kwa mikwaju ya
penalti na Simba wakashinda 5-4.
Oktoba 24, 2007, Simba 1-0 Yanga
Yanga walijikuta wakifungwa mechi
ya tatu mfululizo na Simba katika gemu za Jamhuri Stadium, Morogoro.
Safari hii walimalizwa na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 32′ kwa kiki ya
chini chini iliyompita goliki, Ivo Mapunda katika ‘ kwapa zake’. Baada
ya kipigo hicho Ivo a aliyekuwa mlinzi wa kulia Shadrack Nsajigwa
wakasimamishwa miezi 6 na klabu yao.
April 27, 2008, Yanga 0-0 Simba
Simba ilifikisha gemu ya 15
mfululizo pasipo kupoteza mbele ya mahasimu wao kwa kulamisha
suluhu-tasa. Hadi kufikia gemu hii, Simba ilikuwa imeshinda mara 7 mechi
nyingine zilimalizika kwa sare.
No comments:
Post a Comment