KLABU
itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano kwa
kila mchezaji itakayemsajili mpaka Agosti 30.
Kauli hiyo
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekuja baada ya dirisha la usajili kusogezwa
toka Agosti 6 hadi Septemba 20.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa
Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema pia mwisho wa kufanya uhamisho wa
kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni Septemba 6.“Kikao cha kamati ya sheria kitakaa Agosti 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena Septemba 8 kwa ajili ya kupitisha usajili pia kuanzia Septemba 21- 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi”, alisema Kizuguto
Pia alisema Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Septemba 12, 2015, Daraja la kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
Wakati
huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limesema kuwa bado linaendelea na mazungumzo na wadhamini wa
michuano ya Coca-Cola hivyo ratiba ya michuano hiyo itachelewa kutoka.
Hivyo, inawaomba
kuwa na uvumilivu wakati mchakato wa mazungumzo hayo yanayokaribia ukingoni
ukiendelea.
No comments:
Post a Comment