JUMLA ya
timu 60 zinatarajiwa kuoneshana umwamba kwenye kombe la chama cha soka nchini
linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba mwaka huu.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF)
Baraka Kizuguto alisema kombe hilo ambalo ni maarufu kama kombe la Shirikisho
litazikutanisha timu zinazocheza ligi daraja la pili, daraja la kwanza na ligi
kuu.
“Kombe la
shirikisho litachezwa kwa mtindo wa mtoano na bingwa ndiye atawakilisha nchi
kwenye kombe la shirikisho barani Afrika”, alisema Kizuguto
Pia endapo
itatokea bingwa wa kombe la Shirikisho akaibuka bingwa ligi kuu basi mshindi wa
pili wa kombe la shirikisho ndie atachukuliwa kuiwakilisha nchi kwenye
mashindano ya kombe la shirikisho ambalo misimu iliyopita mshindi namba mbili
wa ligi kuu ndiye alikuwa anaiwakilisha nchi.
Timu
zitakazo shiriki ni 16 ambazo zinacheza ligi kuu na 24 za daraja la kwanza na
24 pia zinazocheza ligi daraja la pili.
Pia amezivitaka
klabu zote kujiandaa vizuri kwani ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa mtoano.
Kizuguto
alimalizia kusema TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wa wachezaji na
viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha leo saa sita usiku kwani baada ya
kufungwa kwa usajili hakutakua na muda tena wa nyongeza.
No comments:
Post a Comment