KAMATI ya uchaguzi ya Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA)
imeitaka kamati ya uchaguzi ya TEFA kufanya uchaguzi wa viongozi, Agosti 23, kama
ilivyopangwa
Akizungumza na wandishi wa habari, msemaji wa DRFA, Omar Katanga
alisema awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike jumapili iliyopita katika ukumbi wa
JKT Mgulani lakini uliahirishwa wanachama wakiwa ukumbini.
“Kamati inapenda kuutarifu umma kuwa mchakato wa ucaguzi una
baraka zote kutoka TFF, hivyo uingiliaji wowote unakwenda kinyume na ibara ya
6(1)ya kanuni za uchaguzi za TFF 2013 na ibara za 52(6) na 56(6)(a) za katiba
ya TFF ambazo zinaelekeza kuwa majukumu ya uchaguzi yapo chini ya kamati ya
uchaguzi”, alisema Katanga.
Itakumbukwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jumapili iliyopita na uliahirishwa
na kamati ya uchaguzi ya Tefa licha ya TFF kuagiza ufanyike hivyo mwenyekiti wa
kamati ya uchaguzi DRFA wakili, Rashid Saadallah akaitaka kamati hiyo ya TEFA
kumuandikia barua kueleza sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.
baada ya kupitia sababu hizo,ndipo DRFA ikatoa majibu kwa
kuelekeza uchaguzi huo kufanyika jumapili hii.
Pia Katanga alisema kozi ya ukocha leseni C inatarajiwa kufanyika
kuanza Agosti 28, katika ukumbi wa TFF, Uwanja wa Karume na washiriki
wanakumbushwa kulipia ada za ushiriki ambayo ni shilingi 250,000.
No comments:
Post a Comment